Mamboleo Mshairi X Leteipa the King – Kumekucha Lyrics

Mamboleo Mshairi X Leteipa the King – Kumekucha Lyrics
#INTRO
Iyeiyeeaaah
Uwouwouwooooh
Lalalalalalalalalalaaaaaa

#CHORUS
Kumekucha waambie
Waskie
Usisitize ili wayaskie
Wasichana wa Afrika
Tujivunie
Ukeketaji nao tuutupilie
Kumekucha waambie
Waskie
Usisitize ili wayaskie
Wasichana wa Afrika
Tujivunie
Ukeketaji nao tuutupilie

Kumekucha
Tuwafwate ili kuwaokoa
Na kuwakomboa
Kama una mawazo ya zamani
Sasa toa,
Kumekucha
Jifunue blanketi ulilojifunika
Blanketi lililokutia kwenye giza
La kuwakeketa
Giza lililowanyima Raha
Na urembo wao wa kumeremeta
Kumekucha
Amka kabla jamii yetu
Itiwe makucha
Tunajua hii ni Mila ya zamani
Ila sasa Haina dhamani
Zamani ilikuwa kwao ni hatari
Lakini sasa kwa wasichana wetu
Ni hatari
Na wanasema
Zoa mchele kabla ndege
Hawajadona
Hebu ona,
Ona maelfu wanavyoangamia
Kwa kumwaga damu
Ona magonjwa yanavyozagaa
Kwa ukeketaji
Kama bado hujaona
Hutaona
Ila waambie,
Kumekucha

Lyricsbyletras.com

#CHORUS
Kumekucha waambie
Waskie
Usisitize ili wayaskie
Wasichana wa Afrika
Tujivunie
Ukeketaji nao tuutupilie
Kumekucha waambie
Waskie
Usisitize ili wayaskie
Wasichana wa Afrika
Tujivunie
Ukeketaji nao tuutupilie

#CHORUS
Mnavyozidi kuwakeketa
Ndivyo jamii yetu inazidi kuchomeka
Tunavyozidi kuwalazimisha wao kuoleka
Kwa wazee waliozeeka
Ndivyo jamii yetu inazidi
Kubomoka tulikoezeka
Simama Leo
Kuwa mwangaza unaoangaza
Kwani,
Taa huwashwa ili kuwekwa peupe
Kumekucha
Tazama uzazi unavyokuwa kazi
Tazama magonjwa kama Fistula
Yanavyotisha kuwala
Kumekucha
Machozi yao kwangu
Nikama kwaruzo la pini
kwenye ini
Damu yao itaturudia
Kama mizimu ndotoni mwetu
Uwepo wao utatoka
Vijijini mwetu
Najua jamii zetu
Na tamaduni zetu
Ni tamu kama asali
Lakini kunazo ambazo Zina uchungu
Wa pilipili
Kumekucha

#BRIDGE
Leo ni Leo
(Kumekucha )
Leo ni Leo
(Kumekucha )
Leo ni Leo ooooh
(Kumekucha )
(Kumekucha )
Leo ni Leo
(Kumekucha )
Leo ni Leo
(Kumekucha )
Leo ni Leo
(Kumekucha )

#VERSE
Tuungane nchi na nchi
Gambia Hadi Zambia
Tanzania wenye nia
Libya walete sura mpya
Nigeria na Algeria
Maanake
Pamoja tunaweza kumaliza ukeketaji
Wa mtoto wa kike
Leo ni Leo
Kumekucha

Search music video on youtube:

    Descubra mais sobre LyricsByLetras

    Assine agora mesmo para continuar lendo e ter acesso ao arquivo completo.

    Continue reading